Genesis 11:10-26

Shemu Hadi Abramu

(1 Nyakati 1:24-27)

10 aHivi ndivyo vizazi vya Shemu.

Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi.
11Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

12 bWakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela. 13Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

14Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi. 15Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

16Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. 17Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

18Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu. 19Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

20 cReu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. 21Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

22 dSerugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. 23Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

24 eNahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. 25Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

26 fTera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani.

Copyright information for SwhNEN